1Ee binti wa mwana wa mfalme, tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu! Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani, kazi ya mikono ya fundi stadi.
2Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa. Kiuno chako ni kichuguu cha ngano kilichozungukwa kwa yungiyungi.
3Matiti yako ni kama wana-paa wawili, mapacha wa paa.
4Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu. Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni karibu na lango la Beth-Rabi. Pua lako ni kama mnara wa Lebanoni ukitazama kuelekea Dameski.
5Kichwa chako kinakuvika taji kama mlima Karmeli. Nywele zako ni kama zulia la urujuani; mfalme ametekwa na mashungi yake.
6Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza, ee pendo, kwa uzuri wako!
7Umbo lako ni kama la mtende, nayo matiti yako kama vishada vya matunda.
8Nilisema, “Nitakwea mtende, nami nitayashika matunda yake.” Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu, harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa,
9
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).
10Mimi ni mali ya mpenzi wangu, nayo shauku yake ni juu yangu.
11Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, twende tukalale huko vijijini.
12Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.
13Mitunguja hutoa harufu zake nzuri, kwenye milango yetu kuna matunda mazuri, mapya na ya zamani, ambayo nimekuhifadhia wewe, mpenzi wangu.