1Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu.
2Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake.
5Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu.
6Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,
7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo,
8msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya kule Meriba, kama mlivyofanya siku ile kule Masa jangwani,
9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.
10
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).
11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.”