1Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu?
3Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa.
4Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika.
6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).