1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali.
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?
4Geuka Ee Bwana, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa kuzimu?
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha nafurikisha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha viti vyangu vya fahari kwa machozi.
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.
9Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, Bwana amekubali sala yangu.
10
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).