1Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili.
2Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3“Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu:
4sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia,
5mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
6Tulisikia habari hii huko Efrathi, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:
7“Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;
8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako.
9Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”
10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).
12kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.”
13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake:
14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku:
15Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula.
16Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.
17“Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu.
18Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”