1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.
3Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.
5Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.
6Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.
7Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.
8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).