1Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa:
2kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia,
3wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai,
4mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika,
5maji yaendayo kasi yangalituchukua.
6Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
7Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka.
8Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed under CC BY-SA 4.0 (creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0).